WHO: Huenda kusiwe na tiba ya haraka ya ugonjwa wa Covid-19
Shirika la Afya Duniani WHO limeonya leo kuwa licha ya kuwepo matumaini makubwa ya chanjo ya virusi vya corona, huenda kusiwe na tiba ya haraka ya ugonjwa wa Covid-19 na kwamba itachukua muda mrefu hadi hali irudi kuwa ya kawaida.
Kulingana na takwimu za shirika la habari la Reuters, zaidi ya watu milioni kumi na nane kote duniani wameambukizwa virusi hivyo na karibu laki saba wamefariki dunia.
Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amezitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kiafya za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo kama uvaaji wa barakoa, kuweka umbali wa mtu na mtu, kuosha mikono na kupima virusi hivyo.
Katika wiki moja iliyopita, tumeona nchi kadhaa ambazo zilikuwa zinaonekana kana kwamba zimepita kile kipindi kibaya zikipambana na ongezeko la maambukizi. Ingawa tumeona pia nchi zengine na maeneo ambayo yalikuwa na kiasi kikubwa cha maambukizi zikifanikiwa kudhibiti maambukizi.”
Mkuu wa masuala ya dharura katika shirika hilo la afya duniani Mike Ryan amesema nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi zinastahili kujiandaa kwa mapambano makubwa.
Mkuu wa masuala ya dharura katika shirika hilo la afya duniani Mike Ryan amesema nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi zinastahili kujiandaa kwa mapambano makubwa.
Comments
Post a Comment