Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Ayoub John mwenye umri wa miaka 38, Mvuvi katika Kisiwa cha Chakazimbwe wilayani Muleba, kwa tuhuma za kumuua kwa kumchinja mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi, amesema kuwa mtoto huyo wa kiume Aidan Greyson alichinjwa na Baba yake wa kambo usiku baada ya kutokea ugomvi baina ya wanandoa hao, uliosababisha mama wa mtoto huyo Mektirida Nestory mwenye umri wa miaka 27 kukimbia kwa kuhofia maisha yake na kuacha mtoto ndani.
Aidha kamanda huyo amesema kuwa Jeshi hilo linawasaka watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Rwegoshora Leonce mwenye umri wa miaka 55 kwa kumpiga na silaha za jadi, ikiwamo fimbo baada ya kumtuhumu kuiba mkungu mmoja wa ndizi wenye thamani ya shilingi 5,000 kutoka katika shamba la Nassib Abdalah, mkazi wa kitongoji cha Kakiri, Kijiji cha Kijongo, Bukoba vijijini.
Chanzo Eatv.tv.
Comments
Post a Comment