Kenyatta Ataka Mawaziri Kuchukua Likizo ya Lazima

 

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka mawaziri wote pamoja na makatibu katika wizara kuchukua likizo ya mapumziko ya lazima huku kukiwa na taarifa za mabadiliko kwenye baraza la mawaziri.

 

Amesema kuwa mawaziri na makatibu watalazimika kushughulikia majukumu ya dharura.

 

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na mkuu wa utumishi wa umma, Joseph Kiyua, likizo hiyo ya siku 11 itaanza Agosti 17 hadi agosti 28, mwaka huu ambapo mawaziri hawatafanya ziara za kukagua miradi na mipango ya serikali.

 

Likizo hiyo  inakuja huku kukiwa kuna taarifa kuhusu  Kenyatta kulifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.

Comments