Mama ajifungua watoto watano kwa mpigo Somalia




Mwanamke mmoja jijini Mogadishu, Somalia amejifungua watoto watano kwa mpigo. Mama na watoto wake wote wanaendelea vizuri japo bado wamelazwa kwa uangalizi zaid wa afya zao.

Taarifa za tukio hilo la nadra zimetolewa na hospitali moja jijini humo ambapo watoto hao wamezaliwa.

Taarifa juu ya utambuliso wa mama na jinsia za watoto hao bado hazijawekwa wazi. BBC inafuatilia taarifa hii na tutakujuza zaidi katika taarifa zetu zijazo.
FUATILIA ZAIDI HAPA>>>> https://www.bbc.com/swahili/live/habari-53647060

Comments