Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amemkabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa UMD, Khalfan Mohamed Mazurui na Mgombea Mwenza, Mashavu Alawi Haji katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma Agosti 10, 2020. Chama hicho kinakuwa cha kumi na mbili (12) kuchukua fomu.
Baada ya kukabidhiwa fomu hizo,Mazururi amesema lengo la chama chake ni kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo, maisha laini, na siyo maisha magumu kama ugali ambao umelala.
Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25, 2020.
Comments
Post a Comment