NEC Yataka Wasimamizi Uchaguzi 2020 Kutozima Simu


WASIMAMIZI wa uchaguzi wa mikoa na wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya wilaya na majimbo, wameagizwa kuhakikisha simu zao zinakuwa wazi katika kipindi chote hadi uchaguzi utakapomalizika na matokeo kutangazwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kadhalika, NEC imewasisitiza wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo kutoka Shinyanga na Simiyu, wakasimamie vizuri uchaguzi huo ili ufanyike huru na haki, bila ya kusababisha dosari zozote zile ambazo zitaleta vurugu na kuchafua amani ya nchi.

Marufuku ya wasimamizi kutozima simu ilitolewa jana mjini Tabora na Ofisa wa NECEdward Makono, wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi 110 kutoka mikoa na Kigoma na Tabora.

Alisema lengo la kuwataka simu zao kuwa wazi ni kuhakikisha kuwa wanakuwa tayari kila wakati kupata maelekezo yanayohusu masuala ya uchaguzi na upokeaji wa vifaa vya uchaguzi vitakapoanza kugawiwa katika maeneo mbalimbali wanayosimamia.

Alisema kitendo cha kuzima simu kinaweza kusababisha msambazaji wa vifaa vya uchaguzi kuchelewa kufika katika vituo vinavyofuata, hivyo kuchelewesha uchaguzi.
Makono alisema msimamizi yeyote ambaye atasababisha vifaa vichelewe kupokelewa kutokana na simu yake kutopatikana, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa umma na za NEC.

Comments