Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema taifa hilo litaondoa marufuku yake inayotokana na virusi vya corona dhidi ya uuzaji wa bidhaa za pombe na tumbaku wiki ijayo huku akitangaza kuondolewa kwa takriban vikwazo vyote katika shughuli za kiuchumi.
Marufuku hiyo inayohusishwa na virusi vya corona katika ununuzi wa pombe na sigara imekuwa na utata na hakuna nchi nyingine iliyoweka vikwazo hivyo kwa pamoja.
Marufuku hiyo iliwekwa wakati Afrika Kusini ilikuwa chini ya amri kali ya kitaifa ya kusalia majumbani mnamo Machi 27 ili kukabiliana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Uuzaji wa pombe ulikatazwa ili kupunguza shinikizo dhidi ya hospitali na kuwaruhusu madaktari kati wadi za kukabiliana na hali za dharura kuangazia ugonjwa wa COVID-19 badala ya ajali za barabarani na majeraha mengine yanayosababishwa na ulevi.
Uuzaji wa bidhaa za tumbaku ulizuiwa kwa sababu ya athari za uvutaji wake pamoja na maambukizi kati ya watu wanaotumia sigara pamoja.
Comments
Post a Comment