Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. John Pombe Magufuli, leo Jumatatu, Agosti 17, 2020, amekabidhi Uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi katika Mkutano wa 40 wa SADC unakaofanyika kwa njia ya video conferencing.
“Jumuiya yetu imepoteza viongozi kadhaa akiwepo Hayati Mkapa, Hayati Robert Mugabe hivyo kabla ya kuanza hotuba yangu tusimame na kuwakumbuka Viongozi hawa. Nizipongeze nchi zote za SADC kwa njia mbalimbali walizochukua kukabiliana na UGONJWA huu wa corona. naamini muda so mrefu tutaondokana kabisa na UGONJWA huu.
“Nichukue nafasi hii kuziomba nchi zilizoendelea kutoa misamaha ya kodi ili kuziwezesha mchi Maskini kuweza kukabiliana na janga hili la COVID19. Moja ya jambo kubwa katika Jumuiya yetu ni usalama, napenda kuwaambia kwamba hilo tumefanikiwa, niwapongeze viongozi wenzangu wa SADC kwa kulisimamia hilo.”
“Wananchi wetu bado ni maskini, wakikabiliwa na changamoto za migogoro, na hiyo inatukumbusha kuwa tukishikamana tunaweza kumaliza changamoto hizo. Ninapokabidhi uenyekiti kwa ndugu na marafiki zetu wa Msumbiji, sisi Watanzania tunafarijika sana kuona kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita tumeweza kutoa mchango wetu ambao bila shaka utakuwa umesaidia kuisogeza mbele SADC.
VIDEO>>>>>
Comments
Post a Comment