TUNDU LISU APOKELEWA KWA KISHINDO ARUSHA



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Antipas Lissu amepokelewa kwa shangwe jijini Arusha katika moja ya ziara zake za mikoani ya kutafuta wadhamini.

Tundu Lisu alifika Arusha juzi tarehe 16 August na kupokelewa na umati mkubwa wa wafuasi wake huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifu wa ushujaa wake.

Akiwahutubia wakazi wa jiji hilo, Lissu alisema njia ya kwenda Ikulu ni nyeupe kabisa sambamba na kuwataka wafuasi wa chama hicho kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.


TAZAMA VIDEO HAPA>>>

Comments